Monday, July 30, 2018

UWEZESHAJI WA VIJANA JUU YA MKAKATI WA USHIRIKI KWENYE KILIMO

Shirika la Door of Hope to Women and Youth Tanzania, DHWYT, kwa kushirikiana na ANSAF pamoja na AMSHA tumeandaa warsha maalumu ya Kuwajengea uwezo vijana juu ya Mkakati wa Taifa wa ushiriki wa Vijana katika Kilimo 2016-2021.
Malengo ya Warsha ni kuongeza uelewa katika sekta ya kilimo kwa ujumla, kuwawezesha vijana kutambua fursa mbalimbali za kilimo zinazopatikana katika kanda ya kisini pamoja na kuwaungaunganisha na wadau wa kilimo waliopo katika maeneo yao, na kuweza kufanya utetezi na ushawishi kwa serikali juu ya mazingira bora ya kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika kilimo.
Waliowezesha ni Vijana kutoka wilaya za Lindi na Mtwara wanaofanya kazi za kilimo, Maafisa Kilimo na Maendeleo ya Jamii, Vijana kutoka kamati za Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa jamii, Waandishi wa habari wa vyombo vyote, pamoja Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali.
Mafunzo ni ya siku mbili, kwa kanda ya Kusini.

Afisa kutoka shirika la AMSHA akiwasilisha taarifa juu ya programu zinazotekelezwa na shirika hilo zinazolenga kuwawezesha vijana wa Mkoa wa Lindi kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kilimo Biashara. 

Afisa Mtendaji wa Kata ya Chuno Wilaya ya Mtwara akichangia juu ya fursa na changamoto za vijana kushiriki kwenye shughuli za Kilimo

No comments:

Post a Comment

MKURUGENZI WA DOOR OF HOPE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MHE. WAZIRI MKUU WA TANZANIA

Katika jitihada za kushirikisha wadau na viongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Watanzania kazi na programu zinazotekelezwa na Shir...