Wanawake ni wengi sana nchini Tanzania; Wakiamua leo kufanya maamuzi sahii, nchi yetu inaweza kupaa katika nyanja zote za kimaisha; yaani kiuchumi, kijamii, kisiasa(demokrasia) n.k
Ni ukweli ulio wazi kwamba pamoja na wingi wa wanawake na wasichana bado mchango wao umekuwa mdogo kuleta mabadiliko chanya kwani ndio wingi wao huo huo umekuwa unaamua na kuchagua viongozi dhaifu/ wasiofaa kwa maendeleo katika maeneo yetu, na Tanzania kwa ujumla. Hii imekuwa ni changamoto kubwa sana na imekuwa ikidhoofisha demokrasia nchini na misingi yake.
Ikumbukwe kuwa elimu ya uraia ni haki ya kila mwananchi(Mtanzania) na inamuezesha na kumuongezea ufahamu, maarifa juu ya masuala ya umma; mfano jinsi ya kuchagua na kuwapata viongozi bora wanaoweza kuleta maendeleo. Elimu hii imekuwa haitolewi kwa wananchi na hasa wale wa vijijini.
Wanawake waliowengi wamekuwa wakichakua bila hiari yao, wamekuwa wakichagua kwa misukomo flani flani, zawadi ndogo ndogo, pesa, pombe(10,000/=), vitenge, kanga, madela,sukari au vyakula n.k ,
hii ni hatari kwa nchi yetu, kiasi kwamba matatizo ya nchi hii tuliyonayo sina shaka kwamba wanawake na wasichana wamechangia kwa kiasi kikubwa sana. Hata hivyo ni matamanio yetu kuona tatizo hili linaisha kabisa mwaka huu kwa wadau na watu binafsi kuendelea kutoa elimu na ufafanuzi juu ya jambo hili hatali kwa mstakabali wa nchi yetu.
Ikumbukwe pia kuwa ni wanawake hao hao wamekuwa wakilalamika juu ya huduma mbaya za afya, maisha magumu, maji, n.k bila kukumbuka kuwa zawadi walizozipokea wakati kama huu ndio maendeleo na huduma zao.
Rai yangu kwa wanawake na wasichana nchini, ni wakati wenu kulivusha taifa letu hapa lilipo, ni wakati wenu kupunguza vilio, ni wakati wenu kuonyesha watanzania na dunai kwamba kura yenu inathamani.
Siku zote rushwa na zawadi vinapofusha na kupumbaza, kamwe usipokee rushwa na ukaishia kufanya maamuzi yasiyo kuwa sahii.
Kudanganywa kila mwaka, kurubuniwa, kutumiwa vibaya na wakati mwingine kutishwa ni matokeo ya wananchi kutojua thamani yao katika uongozi na kuchagua.
KURA YAKO NI MAISHA YAKO KWA MIAKA 5 (Chagua kucheka au Kulia)
No comments:
Post a Comment