Monday, July 30, 2018

MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI KWA WATOTO WA KIKE TANZANIA -

Mkurugenzi Mtendaji wa Door of Hope to Women and Youth Tanzania jana 19/7/2018 alipohojiwa na mwandishi wa habari Ofisini kwake makao Makuu ya DHWYT kuhusu kiwango cha tatizo la Mimba na ndoa za utotoni nchini Tanzania alisema yafuatayo: -
1. Tanzania ni nchi ya 3 kwa tatizo la ndoa za utotoni kwenye jumuiya ya Afrika Mashariki. Ikitanguliwa na Sudani ya Kusini na Uganda πŸ‡ΊπŸ‡¬.
2. Kwa sasa msichana 1 kati ya 5 anaolewa chini ya miaka 18.
3. Kwa Tanzania πŸ‡ΉπŸ‡Ώ kiwango cha watoto wa chini ya miaka 18 wanaoozeshwa ni asilimia 31.
4. Mkurugenzi anasema Wasichana kutoka familia masikini wamo katika hatari ya kuolewa mapema mara 4 zaidi ya wasichana wanaotoka familia tajiri.
5. Pamoja na tatizo hili kichangiwa na kuporomoka kwa maadili na malezi duni kwa watoto kwenye familia nyingi, sababu nyingine ni umasiki kwenye kaya na familia.
6. Akitoa mfano wa kiwango cha tatizo, amenukuu ripoti ya Save the Children na kusema 37% ya wanawake Tanzania walio na umri kati ya 20-24 wameolewa kabla ya kutimia miaka 18.
7. Ametaja sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kuwa na mapungufu na kifungu cha 13 cha sheria hiyo kinaruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 14.
8. Mkurugenzi amesema wasichana wanaoolewa katika umri huu mara nyingi wanakabiliwa na unyanyasaji wa majumbani sambamba na kutengwa na jamii huku wakipewa nafasi ndogo kwa ajili ya elimu na Ajira.
9. Ameonyesha tatizo hili kukidhiri kwenye mikoa ya Lindi, Mtwara hasa Tandahimba na Shinyanga - kwa kanda ya ziwa.
10. Kati ya hatua zinazochukuliwa na shirika kupambana na hali hii ni pamoja na kuwezesha wanawake kwenye kaya mbalimbali kiuchumi ili kupunguza tatizo la Umasikini unaopelekea watoto kukosa huduma za msingi na kujihusisha na matendo/mahusiano ya hatari kama mapenzi n.k
11. Mkurugenzi amewasihi wananchi wote na wazazi kuwasaidia watoto wa kike kufikia ndoto zao, na serikali iweke mazingira rafiki kwa wasichana walioko mashuleni wanaokabiliwa na umbali mrefu kwenda shuleni kwa kujengewa mabweni na kuweka mpango wa chakula shuleni.
Tukishirikiana wadau wote tutapunguza tatizo hili kwa asilimia kubwa zaidi. Wadau wa maendeleo, wazazi/walezi, watoto na serikali wote kwa pamoja tutimize wajibu wetu.
#YouthPower
#WomenPower
#VSIpaneldiscussion
#VSIclinics
#Economicstrengthening

Mkurugenzi Mtendaji wa Door of Hope to Women and Youth Tanzania Ndg. CLEMENCE, Clelinus MWOMBEKI


No comments:

Post a Comment

MKURUGENZI WA DOOR OF HOPE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MHE. WAZIRI MKUU WA TANZANIA

Katika jitihada za kushirikisha wadau na viongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Watanzania kazi na programu zinazotekelezwa na Shir...