Shirika la Door of Hope to Women and Youth Tanzania ni miongoni mwa Mashirika yaliyopata fursa ya kushiriki kwenye mchakato wa kupitia na kutoa maoni ya uboreshaji wa sera ya Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali na kupata nafasi ya kuudhuria kikao kazi cha siku mbili Bungeni Dodoma ili kupitia kwa kwa kina pamoja na wadau wengine maeneo ya msingi ya uzingatiaji kwenye utungaji wa sera mpya. Tayari kikao kazi kimemaliza uandaaji wa Rasimu ya Sera tayari kwa kuiwasirisha kwenye Wizara husika kama pendekezo la wadau wa sekta. Kikao hiki kimeudhuriwa na Shirika mbalimbali kutoka Tanzania bara, Maafisa wa serikali, Msajiri wa NGOs na kimendaliwa na Baraza la Taifa la mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NaCoNGO).
![]() |
Pembeni Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la DOOR OF HOPE akifuatilia mjadala kwenye Ukumbi wa BUNGE - DODOMA |

No comments:
Post a Comment