Shirika la Door of Hope to Women and Youth Tanzania kwa kushirikiana na VSO Tanzania wameandaa Mdahalo wa tafakari na majadiliano (Breakfast panel discussion). Mdahalo huu ulilenga kujadili kwa kina maswala ya #WanawakeNaUchumi pamoja na #WanawakeNaAfya. Hii ni mwendelezo na kuenzi siku ya wanawake Duniani.
Mdahalo huu uliwakutanisha wanawake wa Wilaya ya Mtwara, Asasi za Kiraia, Watu kutoka sekta binafsi, Maafisa wa Serikali kutoka idara mahususi, waandishi wa habari na wanafunzi mbalimbali wa shule na vyuo.
Hakuna ukombozi wa mwanamke kiuchumi bila Afya bora.
Hakuna upiganiaji wa haki kwa wanawake bira Afya bora
No comments:
Post a Comment