Tuesday, July 31, 2018

LENGO NAMBA SITA LA MALENGO ENDELEVU YA DUNIA NI MAJI - WIKI YA MAJI NA HUDUMA BORA ZA MAJI NCHINI

Image may contain: 4 people, people smiling, people standing and indoor
Tarehe 16 - 22 march kila mwaka ni wiki ya maji ulimwenguni.

Lengo namba 6 la Malengo endelevu ya Dunia ni Maji safi na usafi wa Mazingira.

Takribani watu Milioni 663 ulimwenguni hawapati na hawana vyanzo vya maji safi. 


Nchini Tanzania, tatizo la maji bado ni kubwa sana na watu wengi hawapati maji na wengine hawana maji safi.

Tukiwa tunaelekea wiki ya maji kesho, leo DOOR OF HOPE tumetembelea uongozi wa mamlaka ya maji safi Mtwara, MTUWASA na kupata nafasi ya kushirikishana namna bora tunaweza kuongeza upatikanaji wa maji, ulindaji wa miundombinu na vyanzo vya maji, na kuwashirikisha wananchi kulinda na kutunza miundo mbinu hiyo.

Pichani ni Mkurugezi wa MTUWASA na ED- DHWYT na maafisa wa shirika.

No comments:

Post a Comment

MKURUGENZI WA DOOR OF HOPE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MHE. WAZIRI MKUU WA TANZANIA

Katika jitihada za kushirikisha wadau na viongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Watanzania kazi na programu zinazotekelezwa na Shir...