Lengo namba 4 la Maendeleo Endelevu ya Dunia ni Elimu.
Elimu ni kipaumbele cha taifa la Tanzania, na nchini Tanzania elimu inatolewa bila Malipo.
Lengo namba nne linaelekeza kila nchi kuhakikisha kupitia rasilimali zake inatoa elimu jumuhishi na bora kwa watoto.
Utafiti uliofanywa na shirika la Door of Hope mwaka 2017 juu ya ufaulu hafifu wa wanafunzi kwenye shule za msingi na sekondari kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi ulibaini tatizo la Njaa kuwa chanzo cha kutofanya vizuri kwenye masomo yao,
Njaa na kukosa chakula inapelekea wanafunzi kutokuwa na utulivu darasani,mauzulio hafifu shuleni, kutoroka, afya mbaya na matokeo yake Kushindwa kwenye masomo.
Leo tarehe 19 machi, 2018 tumekutana na viongozi mbalimbali na wadau wa Elimu wa kata za Majengo na Likombe wakiwemo Madiwani, watendaji, walimu, Maafisa maendeleo, wenyeviti wa mitaa kujadili changamoto na namna ya kuongeza ufaulu kwenye halmashauri ya Mtwara Mikindani.
Tatizo la njaa kwa wanafunzi na uchache wa walimu kwenye shule za sekondari na msingi yamejitokeza mara nyingi kwenye majadiliano.
No comments:
Post a Comment