Katika jitihada za kushirikisha wadau na viongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Watanzania kazi na programu zinazotekelezwa na Shirika la Door of Hope to Women and Youth Tanzania, Mkurugenzi Mtendaji Ndg. CLEMENCE, Clelinus MWOMBEKI, amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Pamoja na mambo mengi waliozungumza, Mkurugenzi amepata nafasi ya kumueleza Waziri Mkuu programu mbalimbali za Uwezeshaji Vijana na Wanawake nchini Tanzania na namna Shirika lilivyokuwa na mpango wa kuwafikia vijana na wanawake wengi wa pembezoni. Lengo la Shirika ni Kuwa na Vijana na Wanawake wa Kitanzania waliowezeshwa, wenye uwezo wa kutumia nguvu na akili zao, kubaini na kutumia fursa za kitaifa kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Kiuchumi na Kijamii. Baadhi ya programu zinazotekelezwa ni pamoja na Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa jamii - moja ya programu inayolenga kukuza ushiriki wa vijana wa wanawake kwenye masuala ya umma na hivyo kuongeza uwazi na uwajibikaji kwenye utekelezaji wa Miradi ya maendeleo inayotumia fedha za umma; programu nyingine ni Uimarishaji wa Uchumi na Ujasiriamali, Elimu ya Uraia, Afya unasihi wa Lishe na Huduma, pamoja na Utawala bora kwenye kwenye usimamizi, uvunaji na utumiaji wa mapato yatokanayo na rasilimali gesi, Mafuta na madini.
![]() |
Mkurugenzi Mtendaji wa Door of Hope to Women and Youth Tanzania Ndg. CLEMENCE MWOMBEKI akifanya mazungumzo na Mhe. Waziri Mkuu kwenye Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. |


No comments:
Post a Comment