#Tandahimba ni miongoni wa Halmashauri Saba 7 zinazonufahika na programu za Door of Hope hapa nchini. Leo mapema Afisa kutoka Door of Hope Madam Christina Sarwatt mepata nafasi ya kutembelea Wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Tandahimba, Ofisi ya Mkurugenzi wa Tandahimba na kufanya majadiliano juu ya namna ya kuwezesha vijana na wanawake na nafasi ya shirika kuwafikia vijana na wanawake katika wilaya hiyo. Madam Christina pia alipata nafasi ya kutembelea kata chache #Nanhyanga na #Nambaho na kufanya mazungumzo na mahojiano kwa njia ya dodoso na vijana, maafisa maendeleo, madiwani, watendaji wa kata na wanawake wenye kata hizo juu ya nafasi zao na kiwango cha ushiriki wa vijana na wanawake kwenye maswala ya Umma kwenye Wilaya ya Tandahimba.
Ukisaidia MWANAMKE umesaidia JAMII, na VIJANA ni nguvu kazi ya TAIFA. TUWAWEZESHE


No comments:
Post a Comment