#LindiMC Afisa kutoka shirika la Door of Hope atembelea Mkoa wa Lindi na Kufanya Mazungumzo na Ofisi ya Katibu tawala Mkoa, Ofisi ya Mkurugenzi wa Lindi Mjini, na Watendaji wa kata kutoka kata kadhaa za Halmashauri hiyo. Mkoa wa Lindi ni miongoni mwa mikoa 5 inayonufaika na program mbalimbali za shirika ikiwemo programu za Uimalishaji wa kipato na Ujasiriamali kwa vijana na wanawake, Programu ya Elimu ya Uraia, Programu ya Vijana na utawala bora wa rasilimali, na programu za ufuatiliaji wa Uwajibikaji jamii.
Lengo ni kuhakikisha vijana na wanawake wa Kitanzania wanawezeshwa na kutumia akili na nguvu zao, kubaini na kutumia fursa za kitaifa kwa ajiri ya maendeleo endeleo ya kijamii na kiuchumi.
Mikoa mingine ni Mtwara, Kagera na Kigoma



No comments:
Post a Comment