Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii/ Social Accoutability Monitoring- SAM ni dhana shirikishi kati ya wanachi na Viongozi wa serikali inayolenga kishirikisha na kukuza ushiriki wa wananchi kwenye maswala ya Umma, hasa kwenye kusimamia upatikanaji na uboreshaji wa huduma za jamii kwa kuimiza uwazi na uwajibikaji na kudai ufafanuzi, uthibitisho, uhalalisho na usahihisho.
Katika picha, kikosi kazi cha Vijana wajumbe wa Timu za SAM ngazi ya kata kwenye wilaya ya Mtwara wakihainisha maswala ya vijana ya kuzingatiwa kwenye mipango na mikakati ya serikali kwenye ngazi ya kata na wilaya wakati wa mgawanyo wa rasilimali. Pamoja na mambo mengine vijana wa Mtwara wamebainisha mbinu za kuhamashisha vijana wenzao kuona umuhimu wa kushiriki kwenye mikutano ya maendeleo ngazi ya Mitaa/vijiji na Vitongoiji.
No comments:
Post a Comment