Thursday, August 2, 2018

"TUWAWEZESHE KWA RASILIMALI ZETU" TRZ"


DHANA YA MPANGO WA UHAMASISHAJI NA

 UKUSANYAJI WA RASILIMALI 2018-2020

"Tuwawezeshe kwa Rasilimali zetu"


Kwa miongo Zaidi ya mitatu idadi ya vijana nchini Tanzania imekuwa ni Zaidi ya asilimila 60, na hivyo kufanya idadi ya vijana kuonekana kubwa Zaidi ya kundi lolote la kijamii, yaani wazee, wanawake, na watoto. Idadi hiyo inaonekana kwenye maeneo yote ya mijini na vijijini, na hivyo kufanya wadau mbalimbali ikiwemo serikali kuhakikisha kundi hili linapewa kipaumbele kwenye maswala yote ya maendeleo ikiwemo uchumi, afya, siasa, utamaduni na maswala ya kijamii. Jitihada za serikali kwa muda mrefu zimekuwa zikilenga kuona vijana wote wanatumika kikamilifu kwa uzalishaji na kuleta tija kwa taifa kupitia uongozi, maswala ya kilimo, Afya na kukuza teknolojia.
Zimekuwepo kauli mbiu na vibwagizo mbalimbali vya kuhamasisha utayari wa vijana kuwajibika na kutumikia taifa kiuzalendo, vibwagizo kama “Vijana ni nguvu kazi ya taifa”, “Vijana ni taifa la leo” hizi zote zimekuwa zikilenga kuwaandaa vijana kujitambua na kuchukua nafasi yao kama kundi muhimu linalotegemewa na taifa kwenye Nyanja zote za maisha ikiwemo ulinzi na usalama wa taifa letu.
Pamoja na jitihada zote, ikiwemo upatikanaji wa sera ya maendeleo ya vijana na mipango mikakati mbalimbali ya vijana na biashara, vijana na utamaduni, vijana na ushiriki kwenye kilimo; bado kumekuwepo na changamoto kubwa hususani kwenye upatikanaji wa ajira kutoka serikalini na sekta binafsi na ukosefu wa mitaji kwa ajili ya kujiajiri.
Kama zilivyo nchi nyingi barani Afrika, Tanzania pia ni nchi yenye asilimia kubwa ya vijana wasiokuwa na kazi rasmi, na wengi wa vijana hao wanapatika vijijini. Ni miaka ya hivi karibuni ya 2000, nchi yetu imeshuhudia umbwe kubwa la vijana wakihama kutoka vijijini na kuhamia mijini kutafuta ajira na huduma nzuri za kijamii. Kwa upande mwingine ukosefu wa ajira kwa vijana umepelekea mchango wa vijana kwenye taifa lao kuwa mdogo na wengine kutokuwa na mchango kabisa kwenye ujenzi wa Taifa. Ni mara nyingi na kwenye maeneo mengi ya Tanzania, Mikoani na wilayani, Mjini na Vijijini tunashuhudia  vijana wengi wakijihusisha na matendo ya hatari kama uzururaji, uvutaji wa bangi, sigara na madawa ya kulevya, wizi, ujambazi wa kutumia silaha, umalaya na ukatili; haya yote yamepelekea vijana kutoaminiwa na kutoshirikishwa kwenye shughuli na masuala mengi ya kijamii na kitaifa. Mfano, ushiriki wa vijana kwenye mipango na mgawanyo wa rasilimali za maeneo yao (Mitaa, kata, wilaya, Mkoa na Taifa). Hali hii imewanyima uwakilishi wenye tija na unaofuata mtiririko kwenye maeneo na ngazi mbalimbali za serikali.
Tukiwa tunashuhudia matendo ya hatari kwa vijana waliowengi nchini, bado tunasikia jamii inalia juu ya maadili duni na ya kutilia shaka juu ya Mavazi, Lugha, na matendo yasiyokuwa na dhamiri iliyohai. Door of Hope to Women and Youth Tanzania (DHWYT), imejizatiti na imejipanga kuendelea na program mbalimbali za kuwawezesha na kuwasaidia vijana kwenye nyanja zote za kiuchumi, Kijamii, Kitamaduni, kisera, na kimfumo. DHWYT siku zote tumeweza kufanya haya yote kwa mafanikio kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa vijana kutoka ndani na nje ya nchi, Serikali ya Tanzania ikiwa ni mdau namba moja. Mbinu ya Utetezi zinatumika kutatua changamoto zote za vijana za kimfumo na kisera, na kwenye changamoto za uelewa(haki na wajibu) na hamasa kwa vijana, mbinu za Mafunzo ya kujengeana uwezo, Makongamano, mikutano, midahalo na uundaji wa vikundi vya vijana wenye mlengo mmoja zitatumika. Programu kama “Elimu ya Uraia, ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa jamii”, “Uimarishaji wa Uchumi na Ujasiriamali”, “Vijana na Maadili ya Jamii ya Kitanzania” pamoja na programu ya “Vijana na Mawasiliano” zimeendelea kutolewa na shirika. DHWYT kama taasisi ya kuwezesha vijana na wanawake nchini Tanzania itatekeleza programu hizi nchi nzima.

KUHUSU “DOOR OF HOPE TO WOMEN AND YOUTH TANZANIA (DHWYT)”

DHWYT ni shirika lisilokuwa la kiserikali lililojipambanua na kujizatiti kufanya kazi ya kusaidia na kuwezesha vijana na wanawake nchini Tanzania. DHWYT limesajiliwa kwa mujibu wa sheria namba 24, ya 2002, na nambari ya usajasili ni 00NGO/0009273; na hivyo kupewa mamlaka ya kutekeleza miradi ya maendeleo ya vijana na wanawake Tanzania bara. Hadi sasa shirika limeweza kuimarisha shughuli za uwezeshaji kwenye wilaya saba ndani ya mikoa ya Lindi, Mtwara, Kagera na Kigoma, na lengo ni kufikia Mikoa yote ya Tanzania bara.
Lengo kuu la taasisi, ni Kuwa na Vijana na Wanawake waliowezeshwa wenye uwezo wa kutumia akili na nguvu zao, kubaini na kutumia fursa za kitaifa kwa ajili ya maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.
Shirika la DHWYT mpaka sasa limeweza kuwafikia vijana na wanawake kupitia programu za *Uwezeshaji wa kiuchumi na ujasiriamali *Ufuatilianji wa Uwajibikaji kwa jamii *Elimu ya Uraia *Afya, Unasihi wa Lishe na Huduma, pamoja na *Utawala bora kwenye tasnia ya uziduaji –gesi, mafuta na madini.
Katika kufanikisha ufikiwaji wa vijana wengi, shirika limekuwa likitumia njia ya kukusanya rasilimali kutoka nje na ndani ya nchi, kwa kuwafikia sekta binafsi,mashirika ya umma, wadau wa maendeleo, vijana na wanawake kuchangia mahitaji na bajeti kubwa ya taasisi.

Tokea uwanzishwaji wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na Asasi za kiraia nchini tanzania pamekuwepo na utegemezi wa misaada na ruzuku za uwanzishwaji, uimarishaji na uendelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa makundi yote ya kijamii, hasa watoto,vijana na wanawake kutoka kwa wadau wa maendeleo wa nje ya Tanzania (Wafadhili na Wabia). Kwa mazingira hayo utelekezaji wa shughuli za uwezeshaji, utetezi na huduma zinategemea hali ya kiuchumi, kisiasa na kidiplomasia kwenye nchi husika. Mpaka sasa asilimia 97 ya pesa zinazoendesha miradi ya maendeleo kwenye programu na miradi ya utetezi, huduma za moja kwa moja na uwezeshaji zinategemea vyanzo ya nje (donors) na hivyo kukosa uendelevu pindi miradi au programu zinapofika mwisho pia kutoweza kutekelezwa pale wafadhili watakaposhindwa kutoa pesa kwa wakati kutokana na ucheleweshwaji au hali ya kiuchumi kwenye nchi wahisani.
Kwa uzoefu na changamoto hizo, Shirika la Door of Hope to Women and Youth Tanzania (DHWYT) linaendesha mpango maalumu wa “Tuwawezeshe kwa Rasilimali Zetu” (TRZ – Program) kama mpango wake wa ukusanyaji rasilimali, Lengo la mpango huu ni Kuhamasisha ushiriki wa watanzania wote waliofanikiwa kuona umuhimu wa kuchangia mipango ya uwezeshaji wa makundi ya pembezoni na hasa vijana, Wanawake, na Watoto. Mpango huu unalenga kuomba Wasanii vijana, taasisi binafsi, taasisa za umma, viongozi wa umma, wafanyabiashara na wazalendo kujitoa na kuchangia gharama za miradi ya kijamii inayolenga kuwasaidia vijana na wanawake kwenye Nyanja za kiuchumi, afya, elimu ya uraia, na ushiriki wa vijana kwenye masuala ya umma.

LENGO KUU LA MPANGO WA “Tuwawezeshe kwa Rasilimali Zetu”

Katika kufanikisha utelekezaji wa programu DHWYT inatekeleza mpango wa TRZ wenye lengo la Kuhamasisha na kukusanya rasilimali fedha na vitu kutoka kwa wadau wa maendeleo wa ndani ya nchi wakiwemo Makampuni, Wasanii na Watu binafsi waliofanikiwa ili kuweza kufanikisha ufikiwaji wa vijana na wanawake wa pembezoni na vijijini.

MALENGO MAHUSUSI

       1. Kupunguza utegemezi wa wahisani wa nje ya nchi

      2.  Kuongeza ushiriki wa watanzania wazalendo hasa vijana kuona umuhimu wa uwezeshaji wa watanzania wenzao kwa rasilimali zetu wenyewe.

    3.  Kufanikisha upatikanaji wa rasilimali kwa asilimia 100 na kuchangia uelewa wa wananchi kwenye kue
ndeleza na kusimamia miradi ya maendeleo

4. Kutoa nafasi kwa serikali, kuona namna inavyoweza kuwa na kikapu cha pamoja cha wadau kuchagia maendeleo ya ndani kama zilivyo nchi nyingine zilizoendelea




































No comments:

Post a Comment

MKURUGENZI WA DOOR OF HOPE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MHE. WAZIRI MKUU WA TANZANIA

Katika jitihada za kushirikisha wadau na viongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Watanzania kazi na programu zinazotekelezwa na Shir...